Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) ameonya kwamba, kusuasua kwa misaada kunaongezeka wakati ambapo idadi kubwa ya watu wanakimbia migogoro, mateso, ukiukwaji wa haki za binadamu, mabadiliko ya hali ya hewa na umaskini mkubwa.
Migogoro imesababisha watu wengi kuyahama makazi yao kwa idadi kubwa.
Wakimbizi milioni 110 na waliohama makazi yao ni idadi kubwa zaidi katika miongo kadhaa,” Filippo Grandi, mkuu wa UNHCR, alisema alipofungua mkutano wa kila mwaka wa shirika hilo.
Tukio hilo la kila mwaka lilianza dakika moja ya ukimya kukumbuka walio poteza maisha katika tetemeko la ardhi la hivi karibuni nchini Afghanistan na shambulizi la Israel, matukio mawili ambayo yalikumba maeneo hayo mawili siku ya Jumamosi na athari mbaya kwa mamilioni wengine.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu idadi kubwa na isiyo na kifani ya wakimbizi katika ripoti ambayo imepewa anwani “Mashtaka Dhidi ya Hali ya Sasa ya Dunia.”
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, takriban watu milioni 110 duniani kote wamelazimika kuacha nyumba na maeneo yao kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vita na migogoro ya ndani.