Takwimu za hivi karibuni kutoka Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF zimeonyesha kuwa kutokana na kuendelea kwa athari za mzozo na mapambano nchini Sudan, watoto milioni 19 nchini humo kwa sasa hawako shuleni, na shule zaidi ya 10,400 nchini kote zimelazimika kufungwa kwa sababu ya vita.
Miongoni mwao, watoto wapatao milioni 6.5 hawawezi kwenda shule kutokana na vurugu za migogoro katika maeneo yao. Watoto zaidi ya milioni 5.5 katika maeneo salama kiasi, bado wanasubiri shule kuanza tena masomo.
Habari zimesema kuwa kabla ya kuzuka kwa mzozo nchini Sudan Aprili 15 mwaka huu, watoto karibu milioni 7 hawaendi shule kutokana na umaskini na machafuko.
UNICEF imeonya kwamba kama mzozo ukiendelea, watoto wote nchini Sudan watakosa elimu katika miezi ijayo, jambo ambalo litawaingiza kwenye hatari zaidi.