Hivi karibuni taarifa iliokamata hisia za wengi ni juu ya mtandao wa wahalifu uliofichuliwa nchini Pakistan ambao wakati mwingine hukata figo za watu bila wao kujua ambapo msako ulikamata watu 8 akiwemo daktari walikamatwa.
Walivuna figo za watu kinyume cha sheria kwa ajili ya kupandikizwa kwa wateja matajiri na kulingana na mamlaka, baadhi ya wafadhili hawakukubaliana na operesheni hiyo.
Mkuu wa serikali ya jimbo la Punjab la Pakistan, Mohsin Naqvi, alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumapili kwamba Dk. Fawad Mukhtar alifanya upasuaji wa kuondoa figo nyumbani kwake na mara nyingi bila idhini ya wagonjwa na wanaofadhili.
kulingana na shirika la habari la BBC Mnamo 2010, uuzaji wa viungo vya binadamu ulipigwa marufuku na sheria nchini Pakistan.
Anayedaiwa kuwa kiongozi wa biashara hiyo Fawad Mukhtar anatuhumiwa kuchukua figo hizo kutoka kwa zaidi ya watu 300 na kuzipandikiza kwenye wateja matajiri.
Kwa matumaini ya kusitisha usafirishaji wa viungo nje ya nchi na wafadhili. wenyewe, madaktari na wafanyabiashara wa kati, mamlaka ilianzisha adhabu kali: hadi miaka kumi jela na faini kubwa.