Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zinazofanya mageuzi makubwa kiuchumi kwenye sera na sheria zake ili kuvutia zaidi mitaji kutoka nje ya nchi.
Rais Samia amesema hayo akihutubia kwenye mkutano kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na India uliofanyika jijini New Delhi, India.
Katika mkutano huo,Rais ameshuhudia kubadilishana kwa hati za makubaliano baina ya Tanzania na india.