Kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI imesema haijaridhishwa na ujenzi wa jengo la stendi ya Igumbilo .
Ni katika ziara ya kamati hiyo ya kudumu ya bunge ili potembelea manispaa ya Iringa na baadhi ya miradi ikiwemo jengo lililopo katika stendi ya Igumbilo ambapo kamati hiyo imekagua na kugundua mapungufu ikiwemo kutokamilika kwa wakati na tiari jengo hilo linavuja pamoja na nyufa kuanza .
“ hatujaridhishwa na jengo hilo kwasababu ya kutokamilika kwa wakati na jengo hilo lakini hata ukiangalia linavuja na jengo hilo tiari nyufa na kuanza kubomoka tena limeshaanza sisi kama kamati ya tamisemi hatujaridhishwa na mradi huu hivyo naamini litafanyiwa kazi madhaifu haya “
Vilevile mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego ameomba shilingi milioni 161 kwaajili ya kukarabati jengo hilo
Hatahivyo kamati hiyo ya kudumu ya Tamisemi ilikuwa na ziara ya kukagua miradi katika manispaa ya Iringa na kamati hiyo ilikuwa ikiongozwa na mwenyekiti Denis Lazaro na makamu mwenyekiti Justin Nyamoga na miradi iliyotembelea ni pamoja na stendi kuu ya mabasi Igumbilo , soko la Mlandege na barabara ya Don Bosco adi Zizi la Ng’ombe.