Wakala wa Misitu Nchini [TFS] Imetoa Tahadhari kwa wananchi hasa wakulima kuwa waangalifu wakati wa kuandaa Mashamba kwani baadhi yao hutumia moto wakati wa kusafisha mashamba na kusababisha majanga ya moto katika misitu na uoto wa asili jambo linalochochea pakubwa mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Mtaalamu wa kufuatilia Moto wa Msituni na kupambana na moto Bi Kekilia Kabarimu amesema katika maadhimisho ya siku ya maafa iliyoanza terehe 9 mpaka 13 October Mwaka huu, Wakala wa Misitu Tanzania [TFS] imeshirikiana na wananchi katika kutoa elimu ili kudhibiti majanga ya Moto ambayo husababishwa na wananchi pindi wanapoaandaa Mashamba jambo ambalo limekuwa ni Tatizo kubwa hapa Nchini.
Amesema wakulima wanapotaka kuandaa mashamba yao wanapaswa kuchukua tahadhari pamoja na vibali vitakavyosaidia kupata ushauri wa kitaalamu endapo kuna changamoto kubwa itakayopelekea majanga ya moto katika misitu na maeneo ya uoto wa asili.
Kwa upande Afisa misitu,Kutoka wakala wa misitu Tanzania (TFS) Bi Maria Mrutu amesema pamoja na kupambana na kuzuia majanga ya moto katika misitu pia wanashirikiana na wanawake katika ufungaji wa Nyuki ingawaje pia wanaume hushiriki suala ambalo limekuwa likitoa fursa za kiuchumi kwa jamii zimazo zunguka maeneo ya hifadhi na mapori Tengefu.
Baadhi ya Wananchi mkoani Manyara wamekiri kuwepo kwa changamoto ya uelewa mdogo wakati wa uandaaji wa mashamba jambo linalopelekea baadhi yao kutumia moto na kusababisha majanga hivyo nakuipongeza (TFS) kwa kufikisha elimu juu ya namna ya kukabiliana na majanga hayo ili kuepuka Matumizi holela ya moto wakati wa uandaaji wa mashamba.