Baadhi ya raia wa Afrika Kusini waliingia katika mitaa ya Johannesburg siku ya Jumatano kuunga mkono watu wa Palestina, huku mzozo mbaya kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas ukiendelea.
Baadhi ya watu walisema wanajiunga katika maandamano hayo ili kuonyesha mshikamano na Wapalestina ambao wamekabiliwa na ukandamizaji wa miongo kadhaa.
“Nilifanya utafiti zaidi na zaidi na nikafikia hitimisho kwamba sio tu kwamba nimedanganywa, na kujieneza mwenyewe, lakini dini yangu ilikuwa ikitumiwa kudhoofisha haki za watu wa Palestina,” alisema mandamanaji Pamela Ngubane.
Waandamanaji nje ya ubalozi mdogo wa Marekani walikosoa uamuzi wa Washington wa kutuma silaha kwa Israel na kutaka balozi wa Israel nchini Afrika Kusini afukuzwe.
Maandamano sawa na hayo yalifanyika mjini Cape Town huku watu wakitoa wito wa kukomesha ghasia.
Maandamano hayo yaliandaliwa na kundi linalounga mkono Palestina BDS (Boycott, Disinvest, Sanctions) ambalo linaendelea kutoa wito wa kususia bidhaa za Israel, kutowekeza na vikwazo dhidi ya nchi hiyo.
Zilifanyika huku jumuiya ya Wayahudi nchini Afrika Kusini pia ikitangaza mipango ya kufanya vikao vya maombi na matukio ya mshikamano wiki hii ili kuunga mkono Israel.
Serikali ya Afrika Kusini siku ya Jumapili ilitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa ghasia kati ya Israel na Palestina.