Mwanamuziki wa Afrobeat maarufu nchini Nigeria Davido amewaonya mashabiki wake kuacha kusambaza picha za zamani za yeye na mkewe,haya yanajiri huku kukiwa na taarifa za mwimbaji huyo kuwakaribisha mapacha na mkewe, Chioma.
Davido alizidisha tetesi hizo baada ya kupost kwenye X mtandao wake rasmi kuwa wiki hii itakuwa wiki bora zaidi maishani mwake.
Ingawa wapenzi hao hawajatangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo kwenye mitandao ya kijamii, picha za Davido na mkewe zimesambaa sana mitandaoni.
Akijibu kuhusu tukio hilo kwenye X wake rasmi Jumatano, Davido alionya umma kuacha kusambaza picha hizo.
Aliandika:
“Acheni kusambaza picha za zamani, asante.”