Waziri wa Nishati wa Israel Israel Katz alisema kuwa hawatasambaza maji wala umeme wowote hadi Gaza hadi watu waliotekwa nyara na Hamas wakati wa shambulio hilo warudi makwao.
“Msaada wa kibinadamu kwa Gaza? Hakuna swichi ya umeme itawashwa, hakuna pampu ya maji itafunguliwa na hakuna lori la mafuta litakaloingia hadi watekaji nyara wa Israeli warudishwe nyumbani,” alisema kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter.
“Ubinadamu kwa ubinadamu. Na hakuna anayeweza kutuhubiria maadili,” aliandika.
tazama pia…