Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema kuwa mtu yeyote anayetukuza jinai za kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas, kutumia alama zake, kuunga mkono mauaji, wito wa vitendo vya uhalifu au kuchoma moto bendera za Israel anaweza kufunguliwa mashtaka nchini Ujerumani.
Akizungumza katika Bundestag, bunge la Ujerumani, Scholz aliapa “kutovumilia kabisa” juu ya chuki dhidi ya Wayahudi na kutoa wito kwa vyombo vya sheria vya Ujerumani kuwajibisha mtu yeyote anayefanya mambo kama hayo “kwa njia zote ambazo serikali yetu ya kikatiba inatoa.”
“Njia hizi ni pamoja na kupiga marufuku vyama na shughuli.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Shirikisho itatoa marufuku kwa shughuli za Hamas nchini Ujerumani,” Scholz aliongeza.
Matamshi ya Scholz yanafuatia picha za mjini Berlin za baadhi ya watu wakisherehekea shambulio la Hamas dhidi ya Israel wikendi iliyopita, ambalo alilitaja kuwa “la kudharauliwa” na “ukatili” – akiongeza “zinapingana na maadili yote ambayo sisi kama nchi tumejitolea.”
Kuhusu ushawishi wa Iran dhidi ya Hamas, kansela wa Ujerumani alisema, “hadi sasa, hatuna ushahidi dhabiti kwamba Iran imetoa msaada madhubuti na wa kiutendaji kwa shambulio hili la kioga la Hamas,” lakini akaongeza “ni wazi kwetu sote kwamba bila msaada wa Irani.