Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official ametoa wito kwa wadau wa sekta ya Utamaduni na Sanaa nchini wafanye kazi hiyo kibiashara ili wanufaike zaidi.
Dkt. Ndumbaro amesema hayo Oktoba 12, 2023 jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini.
Akiwa katika ziara hiyo, amemuagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Bi. Nyakaho Mahemba ahakikishe kuwa anashirikiana na Benki ambazo zinatoa mikopo hiyo kutoa mafunzo kwa wadau hao kabla ya kuwapatia fedha ili lengo la Mfuko huo litimie.