Serikali ya India imekubali kuondoa ushuru wa asilimia 35 kwa korosho iliyobanguliwa kutoka Tanzania iliyokuwa ikitozwa awali kabla ya Mhe. Rais Samia kufanya ziara ya Kikazi Nchini humo.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akizungumza na Waandishi wa habari akiwa nchini India amesema kuwa korosho itakayoondolewa ushuru huo ni ile itakayokuwa ikibanguliwa na kampuni kutoka India iliyopo nchini.
Waziri Bashe amesema ”India ina sheria inayotoza kodi ya asilimia 35 kwa korosho yoyots inayongia kwao ikiwa imebanguliwa. Sasa kuna kiwanda tumefungua cha kubangua korosho na tumekubaliana ile itakayotoka kwenye kiwanda hicho haitakuwa inatozwa kodi kama ilivyokua hapo awali.
Rais Samia amemaliza ziara yake ya siku 4 Nchini India na sasa amerudi nyumbani Tanzania.