Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga ambae alikuwa ni miongoni walioshiriki Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na India ambapo Mkutano huo ulifanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
Lengo la Mkutano huo ulikuwa nikukutanisha Wadau, Viongozi na Wakuu wa Taasisi ikiwa kukuza na kujadili fursa zilizopo pande mbili kati ya Tanzania na India.
Akizungumza na Millardayo.com Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga alielezea yale yaliyojiri kwenye Mkutano huo.
‘Nitoe Shukrani kwa Kiongozi wetu mpendwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan nashukuru kuchukua fursa hii ya kuelezea Safari ya India kiukweli nitaikumbuka sana kuanzia utaratibu wa kutoka na kwenda kwani timu nzima ya wafanyabiashara imepata shule ya kutosha ya kupanua mawazo makubwa vijana wadogo na vijana wakubwa ambao wapo kwenye biashara’- Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Kwangu mimi mambo mengi yamefunguka na nimejifunza na kwa nchi kama ya Tanzania tunaitafuta kuwa na mikutano kama hii na ukiangalia uhusiano uliokuwepo wa muda mrefu kati yetu sisi na India ni wakati wa muafaka wa kufungua sasa misingi ya Ajira na Clouds Media Group ilijikita katika vitu nyanja tofauti, tukianza na nyanja ya Teknolojia kwenye upande wa Digital tumekutana na Makampuni mengi ambayo yameonesha utayari wa kuja kufanya kazi na sisi’-Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Lakini kwa vitengo vingine vya Clouds kama vitengo vya Oil & Gas kwasababu tuna kampuni nyingine inayodili na mambo hayo kwahiyo tumeweza kukutaba na Wadadu wanaodili na waliobebea kabisa kwenye masuala ya Energy pamoja na wadau wengine wanaodili na masuala ya vilimo’– Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Nitoe shukrani za dhati kwa Uongozi mzima wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kufanikisha hili kwa Wadau na Wafanyabiashara katika ziara ile ya India’-Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga