Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maluum Dkt.Dorothy Gwajima amesema tarehe 15 Oktoba kila mwaka Tanzania huadhimisha siku ya kimataifa ya mwanamke anayeishi kijijini ikiwa ni utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa samba 62 lilipitishwa tarehe 18 Disemba 2007.
Serikali imesema kipaumbele chake kwa sasa ni kuhamasisha uwepo wa mifumo itakayoongeza mwitikio wa wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi ikiwemo upangaji na utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao katika nyanja za uzalishaji mazao ya Kilimo,mifugo na uvuvi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa maendeleo ya Jamii,jinsia na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akizungumza kuelekea maadhimisho ya siku ya mwanamke anayeishi kijijini yanayotaraji kufanyika tarehe 15 mwezi huu mkoani Arusha ,wilaya ya Arumeru Katika ksjiji cha Revolosi kwa lento la kutambua jitihada na mchango wa wanawake wanaoishi vijijini hususani katika nyanja za uzalishaji wa mazao ya Kilimo na uvuvi.
Aidha amesema lingo lingine ni kuhamasisha shughuli za wanawake katika uchumi,kushiriki katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneno yao,kujenga uelewa kuhusu fursa za uzalishaji pamoja na kutoa hamsa kwa wanawake na Jamii kuhusu kukubaliana na umasikini ili kuwa na uhakika wa kipato,chakula na malezi katika kaya.