Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema uhaba wa fedha unazuia mwitikio wa kibinadamu wakati mahitaji ya kibinadamu yakizidi kuongezeka nchini Ethiopia.
Katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu hali ya kibinadamu nchini Ethiopia, UNICEF imesema asilimia 72 ya fedha ilizoomba ambazo ni dola za kimarekani milioni 674.3 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa Ethiopia haijatimizwa, huku mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka kwa watu walio hatarini nchini Ethiopia, hususan katika maeneo ambayo ni magumu kufikika.
Shirika hilo limesema, wakimbizi wanaoendelea kuingia nchini Ethiopia na raia wa nchi hiyo wanaorejea kutokana na mapigano nchini Sudan wameongeza shinikizo la ziada la misaada ya kibinadamu katika mikoa ya Amhara na Benishangul Gumuz nchini Ethiopia.