Ofisi ya wakili mkuu wa serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 imeendesha jumla ya mashauri 7, 392 huku ikifanikuwa kuokoa kiasi cha shilingi Billion mia sita na tisa,milioni mia tatu sitini na nane,laki moja na themanini nne elfu,mia tatu sabini na nane na nukta thelathini na mbili . pamoja na Dola za kimarekeni Million thelathini na saba nukta tatu nne fedha ambazo zingelipwa na wadaiwa endapo serikali ingeshindwa kwenye mashauri hayo.
Hayo yamebainishwa mkoani Tanga na mwenyekiti wa baraza na wakili mkuu wa serikali Dkt. Boniface Luhende wakati akifungua kikao cha kwanza cha baraza la pili la wafanyakazi wa ofisi ya wakili mkuu wa serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo amesema kati ya mashauri hayo 7, 255 ni ya madai na 137 ni ya usuluhishi.
Dkt Luhende amesema kati ya mashauri hayo 7350 ni ya ndani na 41 ni ya nje huku ofisi hiyo ikiwa imefanikiwa kumaliza jumla ya mashauri 620 ambapo mashauri 579 yakiwa yamemalizika kwa njia za kimahakama 41 yakimalizika ni kwa njia ya majadiliano ya nje ya mahakama.
Katika kuendelea kutekeleza majukumu ya ofisi hiyo kwa maslahi mapana ya Taifa Dkt Luhende amewaasa watumiahi wote waliopo katika vitengo mbalimbali kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumj yao ipasavyo kwa kuzingatia sheria, uzalendo uandilifu , na kudumisha ushirikiano.
” Nitoe rai kwenu wajumbe na mfikishe salam hizi wa watumishi wengine kuwa tushirikiane kikamilifu tukizingatia uzalendo uandilifu umoja na mshikamano bila kusahau sheria taratibu na kanuni za utumishi wa umma katika kutekeleza vyema majukumu yetu kuendana na bajeti tuliyopatiwa na dhamana tuliyokasimiwa ” alisisitiza Dkt Luhende.
Aidha ameeleza kuwa ofisi ya wakili mkuu wa serikali imefanikiwa na inaendelea kutatua migogoro mbalimbali nje ya mahakama ili kuzidi kuwavutia wawekezaji na wafanyabishara kupitia sekta ya sheria.
“Ili kutambua mchango wa wawekezaji , wafanyabishara pamoja na wawekezaji ofisi imesuluhisha migogoro mbalimbali kwa njia ya majadiliano nje ya mahakama na mabaraza hatua ambayo imesaidia kukuza imani ya wawekezaji na wafanyabiashara kwa sekta ya sheria nchini pia imekuwa moja ya vivutio kwa wawekezaji nchini” alisema.
Ameongeza kuwa ofisi wa wakili mkuu wa serikali inaendelea kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa katika maadhimisho ya wiki ya sheiria nchini ambapo aliwataka kushughulikia notisi za siku 90 zilizotolewa dhidi ya serikali ili kupunguza idadi ya mashauri na kuimarisha utatuzi wa migogoro kabla ya kuwasilishwa mahakamani ambapo katika kutekeleza hilo tayari kwa kipindi cha mwezi january hadi june 2023 tayari notisi 333 zimeshashughulikiwa.
Awali akizungumza makamu mwenyekiti wa baraza hilo kutoka ofisi ya wakili mkuu wa serikali Mark Mulwambo amesema kuwa ili kuboresha utendaji na ufanisi wa majukumu yao kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wamedhamiria kuhakikisha kuwa wanawajengea uwezo kwa kuwapa mafunzo ya kiutendaji watumishi wote pamoja na kuimarisha mifumo ya Tehema nchini.
“Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ofisi ya wakili mkuu wa serikali imejiwekea bipaumbele mbalimbali ikiwemo kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwapa magunzo ya muda mrefu na muda mfupi ya kibobevu katika maeneo maalumu kama sekta ya mafuta na gesi na kuendelea kuimarisha ofisi zetu za mkoa, kuimarisha mifumo ya tehema ikiwa ni pamoja na kuimaruaha usimamizi wa mashauri” alisema Mulwambo.