Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mkoani Manyara leo October 14,2023 ambapo pamoja na mambo mengine amewataka Watanzania kujiuliza maswali matatu muhimu ikiwemo kwamba, Je, wameendelea kulinda amani!?.
“Hatuna budi tujitafakari kama Taifa namna tunavyotekeleza kwa vitendo msingi wa falsafa ya Mwenge wa Uhuru kwa kujiuliza maswali yafuatayo, swali la kwanza, Je ni kweli tumeendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa Kitaifa?, pili Je, tumeendelea kudumisha uzalendo, uadiifu na nidhamu”
“Tatu tujiulize kama kila mmoja kwa nafasi yake anafanya kazi kwa bidii na kushiriki kikamilifu katika kulijenga Taifa tukitambua kwamba kazi ndio kipimo cha utu”
“Maswali hayo ni muhimu sana na hatuna budi kuendelea kujiuliza kama tunataka Taifa imara linalojitegemea”