Imeelezwa kuwa Mkoa wa Geita ni Moja ya Mikoa Michanga inayoshika nafasi ya 7 kwa wingi wa watu ambapo Mkoa wa Geita unatajwa kuwa na wakazi wapatao Milioni 2 laki 977 na 643 na hii ni kwa Mujibu wa Sesa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022 .
Akitolea ufafanuzi katika Warsha iliyokuwa imeandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Katika kuelimisha Makundi mbalimbali Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh.Martine Shigella amesema kwa sensa ya mwaka 2012 Mkoa wa Geita ulikuwa na wakazi wapatao Milioni 1 na Laki 7 hii imechochea kuleta mafanikio makubwa ndani ya Mkoa wa Geita.
“Sensa ya Mwaka 2012 kwa Geita tulikuwa Milioni 1 na kali 7 Maana ake Baada ya Sensa tumeongezeka kwa Milioni 1 na Laki 2 kuongezeka huko si kwasababu tunazaana sana pamoja na kwamba kule katoro Mh.Mwenyekiti kila mwezi wana watoto zaidi ya 1000 wanazaliwq kila mwezi lakini factor kubwa ni shughuli za kiuchumi zilizo katika Mkoa wetu, ” Mh. Shigella.
Shigella amesema Mkoa wa Geita katika kuchangia Pato la Taifa bado unaendelea kushika nafasi ya 7 ambapo amesema kipato cha Mwananchi Mmoja moja ni sawa sawa na Dollah Moja (Tsh.2500) ambapo amesema Bado Mkoa haujafanya vizuri.
Kharid Msabaha ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali amewapongeza Makamisa wa Sensa wote waliofanya zoezi ambalo limesaidia serikali katika kuleta maendeleo kwa Taifa huku akiwashukuru kwa kuhamsasisha matumizi ya Sensa kwa wananchi ambao walikuwa hawafahamu umuhimu wa Zoezi hilo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mh.Constatine Kanyasu amesema zoezi la Sensa linasaidia kuelewa idadi na takwimu ya Mahitaji katika Jamii huku akiitaka Jamii kuendelea kuamini kuwa Miji mingi inayokuwa inatokana na Idadi ya watu waliopo kupitia Sensa ya watu na Makazi .