Katika kuadhimisha na kusherekea Utamaduni wa asili ya Mtanzania, mojawapo ya kabila ambalo linasifika kuenzi mila na desturi hapa nchini ni pamoja na Wahaya kupitia Tamasha la Buhaya Festival.
Tamasha hili kufanyika kwa dhumuni la kujifunza na kusherehekea asili ya Wahaya kutokea mkoa wa Kagera ambapo watu mbalimbali hujitokeza kufurahia utamaduni wa kabila hili linalosifika kwa mambo mengi kuanzia mtindo wa maisha, chakula na hata Mavazi.
Kwa mwaka huu Tamasha la Buhaya Festival litafanyika siku ya jumamosi tarehe 21 Oktoba eneo la Bahari Beach ambapo Profesa Anna Tibaijuka akiwa ni miongoni mwa watakaoshiriki katika Tamasha hilo huku akiwakaribisha Watanzania wote kushiriki na kuenzi utamaduni wa asili ya Mtanzania.