Takriban watu 50 wamekufa maji na 167 hawajulikani walipo baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kupinduka kwenye mto Congo jioni ya siku ya Ijumaa, kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Didier Mbula, waziri wa afya wa mkoa wa Equateur amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, watu 189 wameokolewa na kwamba msako bado unaendelea.
Katika matamshi yake hayo, Waziri Mbule amesema: “Kwa mujibu wa idadi tuliyonayo hadi sasa katika Serikali ya Mkoa, maiti 49 zimeopolewa, 167 hazijapatikana.”
Ajali mbaya za boti hutokea mara kwa mara katika maji ya Congo hususani kutokana na kuwa vyombo vingi vya majini hupakia watu kupita kiasi.
Nchi hiyo ina ina barabara chache za lami katika eneo lake kubwa lenye misitu, na usafiri mkubwa na wa majini.
Naye Naibu Gavana wa jimbo hilo, Taylor Ng’anzi amesema kuwa ajali hiyo imetokea katika mji wa Mbandaka kwenye Mto Congo katika Mkoa wa Equateur watu wasiopungua 49 wamekufa maji na wengine 120 hawajulikani walipo.