Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha tarehe 2 Oktoba kutumwa kwa kikosi cha kimataifa nchini Haiti, kikiongozwa na Kenya lakini vyombo vya sheria vya Kenya vimesitisha uamuzi huu wa kutumwa kwa maafisa hao wa polisi hadi Oktoba 24.
Upinzani ambao uliwasiolisha malalamiko yake mahakamani ukidai kwamba kutumwa kwa maafisa hawa wa polisi ni kinyume na katiba. Tangu wakati huo, serikali imekuwa ikijaribu kuwashawishi wabunge na wananchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani pia alitetea kutumwa kwa maafisa wa polisi, ambao alielezea kama “heshima kubwa kwa Kenya”, akisema Jumapili kwamba Nairobi haitafadhili misheni hiyo.
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa lazima zichukue mamlaka.
Siku chache mapema, mbele ya kamati ya Bunge, alieleza kuwa hata kama Mahakama ingesimamishakutumwa kwa maafisa wa polisi, hilo halingezuia kuendelea kwa maandalizi.
Kutumwa kwa maafisa wa polisi wa Kenya nchini Haiti kumeidhinishwa tu na serikali, lakini ombi hilo linapaswa kuwasilishwa bungeni wiki hii ili kuthibitishwa. Timu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje pia inapaswa kwenda Umoja wa Mataifa kujadili suala hilo.