Jeshi la Israel lilisema Jumanne kwamba takriban Waisraeli 500,000 wamehamishwa na kuyahama makazi yao ndani ya siku 10 tangu shambulio la Hamas Oktoba 7.
“Kuna takriban nusu milioni ya Waisraeli waliokimbia makazi yao wakati huo,” Jonathan Conricus, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF), alisema katika taarifa yake mtandaoni.
Alisema jumuiya zote zinazozunguka Ukanda wa Gaza zimehamishwa, kama vile jumuiya zaidi ya 20 kwenye mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon.
Lilikuwa shambulio baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya miaka 75 ya nchi hiyo.
Msururu wa mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yamesambaratisha vitongoji na kuwauwa watu wasiopungua 2,750, wengi wao wakiwa Wapalestina wa kawaida.
Wengi walikuwa tayari wameondoka eneo hilo baada ya mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvuka mpaka katika siku za hivi karibuni imesababisha vifo vya watu katika pande zote mbili za mpaka unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa kati ya Lebanon na Israel ambazo zimesalia vitani kiufundi.
Wale waliohamishwa wamepata “kimbilio la muda kwa marafiki na familia katikati mwa Israeli”, Conricus alisema.