Rais wa Urusi Vladimir Putin aliwasili Beijing siku ya Jumanne kukutana na mwenzake wa China, Xi Jinping, katika safari iliyotazamwa na watu wengi yenye lengo la kuonyesha kuaminiana kwa kina na ushirikiano “bila kikomo” kati ya China na jirani yake mkubwa.
Putin na wasaidizi wake waliingia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing Jumanne asubuhi, kulingana na picha za video za Reuters, katika safari rasmi ya kwanza ya mkuu huyo wa Kremlin nje ya uliokuwa Umoja wa Kisovieti mwaka huu.
Putin amesafiri kidogo nje ya nchi tangu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yenye makao yake makuu The Hague (ICC) ilipotoa kibali cha kukamatwa kwake mwezi Machi, ikimtuhumu kwa kuwafukuza watoto kutoka Ukraine kinyume cha sheria.
China wiki hii inatarajiwa kuwa mwenyeji wawakilishi kutoka katika mataifa 130 ya dunia, katika kongamano rais Xi kuhusu biashara na miundo mbinu na masuala ya barabara.
Kongamano hili linafanyika wakati huu mapigano yakiendelea kuripotiwa kati ya wanajeshi wa Israeli na wapiganaji wa Hamas.
Rais Putin ni miongoni mwa wageni wa ngazi ya juu kwenye kongamano hilo, hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwenye taifa lenye uchumi mkubwa tangu nchi yake kuivamia Ukraine.
Rais Xi alifungua kongamano hilo siku ya Jumanne kwa kufanya mazungumzo na marais wa Chile na Kazakhstan kwa mujibu wa shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Beijing.