Wanajeshi wa Israel waliwauwa wanamgambo wanne waliokuwa wakijaribu kujipenyeza kutoka Lebanon, jeshi lilisema Jumanne, huku hali ya wasiwasi ikitanda kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
“Muda mfupi uliopita, askari waangalizi wa IDF (jeshi la Israel) waliona kikosi cha magaidi kikijaribu kupenyeza uzio wa usalama wa Lebanon na kutega kifaa cha kulipuka,” jeshi lilisema katika taarifa. “Magaidi wanne waliuawa.”
Hapo awali jeshi lilisema lilifanya mashambulio usiku kucha dhidi ya malengo ya “magaidi” ya Hezbollah ndani ya Lebanon.
Tangu kuanza kwa vita vilivyochochewa na shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba, mapigano kwenye mpaka wa Israel na Lebanon yamesababisha takriban watu 10 kuuawa upande wa Lebanon, wengi wao wakiwa wapiganaji lakini pia mwandishi wa habari wa Reuters na raia wawili.
Kwa upande wa Israel, takriban watu wawili wameuawa.
Jumuiya ya kimataifa inahofia kufunguliwa kwa mkondo wa pili katika mzozo huo, huku kundi la Lebanon la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran likiungana na mshirika wake wa Hamas katika vita dhidi ya Israel.
Sikiliza nyimbo za hivi punde, kwenye JioSaavn.com pekee
Israel imeanza kuwahamisha maelfu ya wakaazi kutoka maeneo 28 kaskazini mwa nchi hiyo.