Marekani siku ya Jumatano ilitoa vikwazo vinavyohusiana na ugaidi dhidi ya watu tisa na taasisi moja yenye uhusiano na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye tovuti yake, hatua za Idara ya Hazina zinalenga wanachama wanaosimamia mali katika “jalada la siri la uwekezaji la Hamas, mwezeshaji wa kifedha wa Qatar mwenye uhusiano wa karibu na utawala wa Iran, kamanda mkuu wa Hamas, na Gaza,ubadilishaji wa sarafu halisi na mwendeshaji wake.”
“Marekani inachukua hatua za haraka na madhubuti kuwalenga wafadhili na wasaidizi wa Hamas kufuatia mauaji yake ya kikatili na ya kiholela dhidi ya raia wa Israel, wakiwemo watoto,” Katibu wa Hazina Janet Yellen alisema.
Hamas ilianzisha mashambulizi ya kushtukiza ndani ya Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua watu 1,400, wengi wao wakiwa raia.
Baada ya Israel kutangaza vita na kuanza mashambulizi ya kulipiza kisasi, karibu watu 3,500 wameuawa katika Ukanda wa Gaza, wengi wao wakiwa ni raia pia, kulingana na mamlaka ya afya ya Hamas.
Zaidi ya wengine 12,000 wamejeruhiwa katika jibu la Israel.