Serikali imewataka Wajasiriamali nchini kushirikiana na Shirika la viwango nchini TBS katika kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha ili bidhaa wanazozalisha ziweze kushindana katika masoko ya kimataifa.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara EXAUD KIGAHE wakati akifungua maonesho ya biashara ya TANZANITE MANYARA TRADE FAIR yanayoendelea katika viwanja vya stendi ya zamani mjini BABATI yaliyoanza tangu tarehe 17 hadi 21 Oktoba.
Akizungumza katika maonyesho hayo Mkurugenzi wa biashara na masoko wa Tracom Fertilizers Ltd Mkoani Dodoma Dr, Kinneth Masuki amewahimiza wafugaji kupata soko la samadi yao katika kiwanda Cha mbolea ya mseto ya chumvi na samadi(FOMI) chenye uwezo wa kuzalisha Tani elfu Moja za mbolea.
Amesema kiwanda hicho kina mitambo mitano ya kuzalisha mbolea yenye ujazo wa Tani laki mbili Kila mtambo “Hiyo ni mbolea nyingi sana inayohitajika katika Kila mtambo ambapo Kwa mwaka zinahitajika jumla ya Tani laki Saba”Masuki
Mmoja wa wakuluma na mkazi wa Kijiji Cha Gallapo wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara Leonard Ngotta amesema Mkulima akilima na kupanda mapema na kutumia mbolea hiyo atakuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TCCIA Manyara Musa Msuya amesema wajasiriamali zaidi ya 1,200 wanaotegemewa kushiriki Maonesho hayo mwaka huu,huku akiishukuru Serikali kwa kukubali kujenga kiwanja Cha ndege Mkoani Manyara jambo ambalo litaongeza idadi ya watalii pamoja na wawekezaji katika mkoa wa Manyara na Taifa kwa ujumla.
Nae Meneja Masoko Kampuni ya Mati Super Brands Ltd Elvis Peter amesema maonyesho hayo yanaunga mkono nia ya Serikali katika kiwasaidia wajasiriamali na wawekezaji nchini katika kukidhi mahitaji ya jamii.