Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 19 Oktoba, 2023 amewasili Jijini Luanda nchini Angola kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 147 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 20 hadi 29 mwezi huu nchini humo.
Mkutano huo wenye dhima kuu kuhusu “Hatua za Kibunge kuchagiza Amani, Haki na kujenga Taasisi Imara” (Lengo la 16 la Maendeleo Endelevu). Katika Mkutano huo pamoja na mengineyo utafanyika Uchaguzi wa Rais mpya wa Umoja huo ambapo Dkt. Tulia ni miongoni mwa Wagombea waliojitokeza katika kinyang’anyiro hicho.