Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa maagizo manne kwa Baraza la wafanyakazi la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ikiwamo kuwasajili waajiri wote chini.
Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo Oktoba 19, 2023 wilayani Morogoro alipokuwa akifungua kikao cha Baraza hilo. Amesema ni muhimu WCF ikaongeza malengo ya kusajili waajiri wote hasa wa sekta binafsi ambao wanaajiri wafanyakazi wengi wa ngazi ya chini na wanaofanya kazi kwenye mazingira hatarishi.
“Suala jingine ni elimu kwa umma huu mfuko ni muhimu unawagusa watanzania wote kutokana na wapendwa wao kupata madhira kazini, wajue manufaa ya mfuko na majukumu yake ,”amesema.
Pia, amehimiza kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ili watanzania wavutiwe na huduma zinazotolewa. “Mmbebe jukumu hili kwa pamoia na kazi hi muibebe kwa movo lakini mkifanyia kwa maslahi hamtafanikiwa,
pia suala jingine ni mashirikiano fanyeni kazi kama timu muheshimiane wafanyakazi na viongozi ili kuleta ufanisi wa mfuko,”amesema.
Naye, Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, amesema mfuko upo imara na wajumbe wa baraza hilo wamejadili masuala mbalimbali ikiwamo huduma za utengamao.