Idadi ya vifo imeongezeka hadi 4,385, huku majeruhi sasa wakifikia 13,651, kulingana na wizara ya afya ya Palestina inayoendeshwa na Hamas.
Waliouawa ni pamoja na watoto 1,756 na wanawake 976, wizara ya afya iliongeza.
Pia ilitoa taarifa ikipinga kutengwa kwa mafuta kutoka kwa misaada ya kibinadamu inayotumwa Gaza.
Ilisema ingeacha maisha ya wagonjwa na waliojeruhiwa hatarini.
“Tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na Misri kufanya kazi mara moja kuleta mahitaji ya mafuta na afya ya dharura kabla ya waathiriwa zaidi kupotea hospitalini,” ilisema taarifa hiyo.