Youcef Atal, mwanasoka maarufu kutoka Algeria na mchezaji wa klabu ya Nice nchini Ufaransa, anaandamwa na wanasiasa wa Ufaransa baada ya kuukosoa utawala wa Israel.
Mwanasiasa Eric Ciotti wa Ufaransa amewataka wanasiasa wenzake kuchukua hatua dhidi ya Atal kwa kukosoa mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wa Gaza.
Anwar El Ghazi, mchezasoka Mholanzi mwenye asili ya Morocco, mkataba wake na klabu ya “Mainz” ya Ujerumani umevunjwa baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumshambulia kwa kuwaunga mkono watu wa Gaza.
Umoja wa Ulaya pia umeondoa picha ya muogeleaji wa Misri, Abdelrahman Sameh, kwenye kurasa rasmi za Umoja huo kwa kuwa na misimamo ya kuwatetea watu wa Palestina dhidi ya ukatili wa Isarel.
Sameh pia amethibitisha kwamba, ametishiwa kuuawa kwa sababu ya kuwaungaji mkono watu wa Palestina.
Mesut Özil, nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu za Arsenal na Real Madrid, anandamwa vikali baada ya kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii ukiwa na bendera za Uturuki na Palestina.