Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi ya anga mapema Jumatatu (Oktoba 23) katika vituo viwili vya Hezbollah nchini Lebanon taarifa zikidai kuwa Seli hizo zilidaiwa kupanga kurusha makombora kuelekea Israel.
Wakati Hezbollah ikikiri kuwa mmoja wa wapiganaji wake aliuawa, maelezo hayakufichuliwa.
Likithibitisha tukio hilo, shirika la habari la serikali ya Lebanon NNA liliripoti shambulio la anga la Israel kwenye viunga vya kusini mwa Aitaroun, lakini halikutoa maelezo zaidi.
Jeshi la Israel lilisambaza picha za mashambulizi hayo, moja likilenga seli karibu na mji wa Israel wa Mattat, takriban kilomita 13 (maili 8) kusini-magharibi mwa Aitaroun, huku shambulio lingine likitokea katika eneo linalozozaniwa la mashamba ya Shebaa. Israel ilidai kuwa ililenga seli zote mbili kabla hazijaanzisha mashambulizi.
Mashambulizi ya ziada ya Israeli yameripotiwa kugonga shabaha zaidi za Hezbollah, ikijumuisha kiwanja na kituo cha uchunguzi, bila ripoti za haraka za majeraha au uharibifu.