Raia wa Gaza wanakabiliwa na “mashine ya mauaji na uhalifu wa Israel”, waziri mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh amedai.
Inakuja wakati Wapalestina 400 waliuawa na mashambulio ya anga ya Israel huko Gaza katika saa 24 zilizopita, kulingana na maafisa wa afya wa Palestina.
Idadi ya vifo, takriban 4,200, inajumuisha idadi kubwa ya wanawake na watoto, pamoja na waandishi wa habari 11 wa Kipalestina, wafanyikazi 28 wa matibabu na wafanyikazi 14 wa UN, kulingana na UN.
Idadi ya waliouawa Israel imefikia 1,400 tangu Oktoba 7, kulingana na maafisa wa Israel.