Wananchi Waislamu wa jimbo la Bauchi nchini Nigeria kwa mara nyingine tena wameandamana na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.
Waislamu hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamesikika wakipiga nara za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wakiwa wamebeba bendera za Palestina, Waislamu hao wamemtaka Rais wa nchi hiyo Bola Ahmed Tinubu kumtimua haraka iwezekanavyo kutoka Abuja balozi wa utawala haramu wa Israel.
Kadhalika waandamanaji hao wameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua zaa haraka za kuhitimisha mauaji na jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.
Baadhi ya waandamanaji hao wamesisitiza kuwa, balozi wa Israel nchini Nigeria ni lazima afukuzwe nchini humo.