Mwigizaji wa Marekani Will Smith amesema ataendelea kumuunga mkono mke wake, Jada Pinkett, kwa “maisha yangu yote” licha ya jada kufichua katiaka kipindi cha mazungumzo kwamba yeye na mumewe wametengana kwa miaka saba sasa.
Hata hivyo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Will alisema Jada ni “rafiki mkubwa zaidi ambaye nimewahi kuwa naye kwenye sayari hii”, akisisitiza kwamba ataendelea kumuunga mkono.
Alifafanua ndoa yao kuwa “jaribio la hadharani la upendo usio na masharti.”
“Muungano wetu ni jaribio la hadharani la upendo usio na masharti. Je, unaweza kumpenda mtu milele, bila kujali nini? Je, unaweza kumpenda mtu kwa maisha yako yote hata kama humkumbuki?
“Jada ndiye rafiki bora ambaye nimewahi kuwa naye kwenye sayari hii na nitamsaidia maisha yangu yote,” AfroNews ilimnukuu Will Smith akisema.