Jeshi la Israel limesema limewakamata watu 64 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan usiku kucha, wakiwemo wanachama 37 wa kundi la kigaidi la Hamas.
Inafikisha idadi ya waliokamatwa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu kufikia 800, wakiwemo zaidi ya 500 wanaoshirikiana na Hamas, Israel ilidai.
Inakuja baada ya Wapalestina wawili kuuawa katika kambi ya wakimbizi ya Jalazone katika Ukingo wa Magharibi, kulingana na wizara ya afya ya Palestina inayoongozwa na Hamas.
Vikosi vya Israel vilivamia kambi hiyo na kutekeleza “kamata kamata nyingi”, ambapo walipambana na watu wenye silaha na vijana waliorusha mawe.