Nchini Liberia, Tume ya Uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 10 Jumanne hii kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani.
Chombo kinachohusika na kuandaa na kutangaza matokeo ya mwisho tayari kimehesabu kura kutoka 99.9% ya vituo 5,890 vya kupigia kura nchini Liberia na Rais anayemaliza muda wake Georges Weah anaibuka kidedea kwa kura ndogo ya 43.84% sawa na kura 803,674 mbele ya Joseph Boakai 43.44 % au kura 796,313 ambazo ni sawa na tofauti ya kura 7,361 au 0.40%. Kulingana na waangalizi wa mambo, hili ndilo pengo finyu zaidi katika historia ya Liberia tangu kumalizika kwa vita.
Hakuna mgombea hata mmoja ambaye ameweza kupata 50% ya kura pamoja na kura moja, tunaelekea duru ya pili, tarehe ya awamu ya pili ambayo itatolewa na Tume ya Uchaguzi.
Na duru hii ya maamuzi inapaswa kuchezwa katika kaunti ya Montserrado ambayo ina karibu kura milioni.
Mgombea mkuu wa upinzani nchini Liberia, Joseph Boakai, anawania vyama vidogo kabla ya duru hii ya pili dhidi ya Rais anayemaliza muda wake George Weah ambayo inapaswa kufanyika Novemba 7, isipokuwa kutakuwa na mabadiliko ya dakika za mwisho.
Georges Weah alishinda uchaguzi wa 2017 kutokana na matumaini makubwa yaliyotolewa na ahadi yake ya kupambana na umaskini na kukuza maendeleo ya miundombinu katika jamhuri kongwe zaidi ya Afrika.
Kwa Davidetta Browne-Lansanah, rais wa NEC, fedha zinazohitajika kwa ajili ya kuandaa duru ya pili ya uchaguzi hatimaye zinapatikana na upigaji kura unapaswa kufanyika bila matatizo makubwa.