Hospitali tatu huko Gaza zimelazimika kufungwa baada ya kukosa mafuta ya kuendeshea jenereta zao za umeme, waziri wa afya wa Palestina amesema.
Mai al-Kaila alisema kuna udharura wa kuanzishwa korido salama ili kusogeza majeruhi na wagonjwa mahututi kupata matibabu katika hospitali za Misri.
Mapema leo, Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema karibu theluthi mbili ya vituo vya afya huko Gaza vimeacha kufanya kazi.
Ilifuata onyo kwamba viwango vya mafuta vilikuwa vikipungua kwa hatari katikati ya vizuizi vya Israeli.