Michuano ya Golf ya NCBA Bank Tanzania Open 2023 baada ya kushindwa kufanyika mwaka jana sasa itafanya mwaka 2023 kuanzia 23-26/11/ katika viwanja vya Kili Golf jijini Arusha taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Golf Club Tanzania.
Ambapo michuano hiyo leo imetambulisha Wadhamini wao waliowaunga Mkono NCBA Bank ambayo iliwakilishwa na Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wao Claver Serumaga pamoja na Vodacom Tanzania ambayo iliwakilishwa na Meneja Masoko wao Bi Irene Neema.
“Nia yetu ni kuanzisha ushirikiano mzuri wadau kama hawa kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa golf, tutashirikiana nao katika mashindano haya lakini wamekitolea kuendeleza mchezo huu kuanzia ngazi za chini zaidi”
Mashindano ya mwaka huu yatakuwa na vipengele viwili professional ambao watacheza na division A kwa siku nne mashimo 72 na wachezaji wa ridhaa ambao watacheza kwa siku mbili tarehe 25-26/11/2023 mashimo 36.