Mwendesha mashtaka ameomba kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kutwaliwa mali yake dhidi ya rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz.
Akishtakiwa kwa kujitajirisha kwa njia haramu, matumizi mabaya ya mamlaka na utakatishaji fedha, Mohamed Ould Abdel Aziz alikuwa amejilimbikizia mali na mtaji wa euro milioni 67 wakati aliposhtakiwa mnamo Machi 2021.
Kesi ya siku ya Jumanne iliyochukua karibu saa tatu ambapo mwendesha mashtaka Ahmed Ould Moustapha alitangaza kwamba “vielelezo vyote vilivyo mikononi mwa ofisi yake vinathibitisha
kuwa rais huyo wa zamani alifanya uhalifu”.
Kwa hiyo aliomba kifungo cha miaka 20 jela dhidi ya rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye anashitakiwa, miongoni mwa mambo mengine, kwa kujitajirisha kinyume cha sheria. Pia aliomba kunyang’anywa mali yake.
“Anastahili hii kwa sababu uhalifu ni mbaya sana na ulio wazi. Ushahidi ni mwingi. Ushahidi wote upo ili apate hukumu ya juu zaidi.
Rais wa Jamhuri anayetumia taratibu kujitajirisha na ambaye anatumia mali ya shirika kwa manufaa ya umma kutengeneza nyumba yake na kununua majengo ni hatia,” anasema wakili Vadili Raiss, Wakili Mkuu wa Serikali.
Mwendesha mashtaka pia aliomba, pamoja na mambo mengine, kifungo cha miaka 10 jela dhidi ya mawaziri wakuu wawili na mawaziri wawili wa rais huyo wa zamani.