Meneja wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe usiku huu amelazimika kwenda Temeke katika godown lililohifadhi shehena ya jezi feki za Simba na Yanga baada ya kusikia mzigo huo unataka kutoroshwa.
Ally akiwa ameambatana na Waandishi wa habari ameiomba serikali iingilie kati suala hilo ili haki itendeke kwani mzigo uliokamatwa untajwa kuwa ni Mabilioni ya Shilingi.
Wakati Ally alipofika eneo la tukio mlinzi wa eneo hilo aliamza kuleta vitisha vya kutaka kumpiga kabla ya baadhi ya watu kumzuia, inasemekana inafanyika njama ya kuondoa mzigo huo.