Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamejadili “juhudi zinazoendelea za kutafuta na kupata kuachiliwa” kwa Wamarekani wanaoaminika kuwa mateka huko Gaza, Ikulu ya White House ilisema.
Bw Biden pia alisisitiza kwa Bw Netanyahu “umuhimu wa kuzingatia kile kinachokuja baada ya mgogoro huu kujumuisha njia ya amani ya kudumu kati ya Waisraeli na Wapalestina”.
Hapo awali, Rais Biden alizungumza dhidi ya mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan baada ya mashambulizi ya Hamas.
Pia alisema anaongeza ahadi yake ya kufanyia kazi suluhisho la mataifa mawili ili kumaliza mzozo wa miongo kadhaa kati ya Israel na Palestina.
Alisema mashambulizi ya “walowezi wenye itikadi kali” ni sawa na “kumwaga petroli” kwenye moto ambao tayari unawaka katika Mashariki ya Kati tangu shambulio la Hamas.
\”Lazima ikome. Inabidi wawajibike. Inabidi ikome sasa,” Joe Biden alisema.