BENKI ya I&M imezindua huduma mpya ya mikopo binafsi isiyokuwa na masharti ikiwamo ada ya mikopo na akaunti tatu mpya za miamala katika kuboresha utoaji huduma kwa wateja wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Zahid Mustafa, akizungumza na waandishi wa habari Octoba 26/2023 jijini Dar es Salaam kuhusu huduma hiyo, amesema watakuwa wa kwanza nchini kutoa huduma bila malipo kwa miamala ya fedha, kutoa fedha taslimu bila malipo kutoka ATM mashine za benki hiyo.
Amesema kutokana na kuwapo kwa ukuaji wa teknolojia ya watu kutumia huduma ya mtandao kutoa fedha, wameona kuzindua akaunti tatu za kutoa fedha bure.
Ametaja huduma hizo kuwa ni kutoa malipo ya bili bila malipo, kadi za debit bure kama sehemu ya bidhaa tatu muhimu ambazo Moja akaunti, Everyday Account’ na ‘Chagua akaunti’
“Tunafuraha kutambulisha huduma hizi za akaunti zilizoboreshwa, kuonyesha dhamira yetu ya kuelewa na kukidhi mahitaji ya kipekee ya wateja wetu wanaothaminiwa. Tunawawezesha wateja kuchagua suluhisho sahihi la kifedha linalolingana na matarajio yao ya miamala,” amesema.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja na Kidigitali, Deepali Ramaiya, amesema, “Maendeleo mapya yanatoa vipengele vingi vilivyoundwa ili kutoa uzoefu usio na mshono wa benki kwa wateja, kuwezesha shughuli zao za kifedha kwa urahisi na amani ya akili.”
Akifafanua kuhusu huduma hizo, amesema Akaunti ya Moja haina makato mengi na yanatokana na matumizi ya akaunti ya mara kwa mara.
Amesema Everyday akaunti kila mwezi mteja anaweza kufanya miamala hadi mitano kwa mwezi mmoja bure na kadi hiyo inatumika bila makato yoyote.
Amesema akaunti ya select ni wateja maalum kwaajili ya kutoa huduma zote bure baada ya kulipia kiasi kidogo wakati wa kuifungua.
Ramaiya amesema pia watatoa mikopo hadi milioni 100 ndani ya saa 24 kwa hadi miaka sita.
“Kupitia msimu huu wa sikukuu tunawapa ofa kabambe ya kutoa mikopo ya bei nafuu yenye riba chini ya asilimia 18 kwa wateja wote bila ada za mikopo kama wewe ni mteja wetu unakaribishwa kupata huduma hii,” amesema.