Beki wa Nice Youcef Atal amefungiwa mechi saba na Ligue 1 kwa chapisho la mtandao wa kijamii kuhusu vita vya Iarael-Hamas, ilitangazwa Jumatano.
Nice ilikuwa tayari imemsimamisha kazi Atal wiki iliyopita hadi itakapotangazwa tena na kusema kwamba aliomba msamaha kwa kitendo chake.
Baada ya suala hilo kukaguliwa na kamati ya maadili ya shirikisho la soka la Ufaransa, tume ya nidhamu ya ligi ya Ufaransa ilimsimamisha kazi Atal.
Kusimamishwa kwa Atal kunakuja baada ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Nice kufungua uchunguzi wa awali ukimlenga Atal kwa tuhuma za “kutetea ugaidi” kwa kusambaza ujumbe huo mtandaoni.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema Atal pia anachunguzwa kwa “uchochezi wa umma kwa chuki au vurugu kwa sababu ya dini fulani.”
Atal mwenye umri wa miaka 27, ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Algeria, aliomba msamaha baada ya kuripotiwa kuchapisha tena na kisha kufuta video ambayo mhubiri wa Kipalestina alitoa kauli ya chuki.
Akiandika kwenye Instagram, Atal alisema anaelewa kuwa chapisho lake liliwashtua baadhi ya watu na kusema analaani aina zote za vurugu, “bila kujali ni wapi duniani.”