Kundi la Hamas la Palestina ambalo linadhibiti Gaza haliwezi kuwaachilia mateka waliokamatwa wakati wa shambulizi lake dhidi ya Israel hadi makubaliano ya kusitisha mapigano yakubaliwe, gazeti la Urusi la Kommersant lilimnukuu mjumbe wa ujumbe wa Hamas unaotembelea Moscow akisema.
Imemnukuu Abu Hamid akisema Hamas ilihitaji muda kuwatafuta wote waliochukuliwa kutoka Israel hadi Gaza na makundi mbalimbali ya Wapalestina katika shambulio la Hamas tarehe 7 Oktoba.
“Walikamata makumi ya watu, wengi wao wakiwa raia, na tunahitaji muda kuwatafuta katika Ukanda wa Gaza na kisha kuwaachilia,” Hamid alisema.