Hamas iko tayari kuwaachilia mateka wake raia kwa sharti kwamba Wapalestina 6,000 wanaozuiliwa katika jela za Israel pia waachiliwe, waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema.
Akizungumza katika mkutano wa dharura wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Hossein Amirabdollahian alisema Iran “iko tayari kutekeleza sehemu yake katika azma hii muhimu ya kibinadamu, pamoja na Qatar na Uturuki”.
Alisema dunia “inapaswa kuunga mkono kuachiliwa” kwa wafungwa wa Kipalestina.
Jeshi la Israel hapo awali liliongeza idadi ya watu wanaoaminika kushikiliwa mateka na wanamgambo huko Gaza hadi 229. Mateka wanne wameachiliwa huru kufikia sasa.