Mamlaka ya usafiri wa anga leo hii wamepokea makontena tisa kwenye bandari ya Dar es salaam yaliyobeba mitambo ya mawasiliano kutoka nchi za Norway na Italy.
Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya usafiri wa Anga Hamza Johari amesema hatua ya kufungwa Kwa mitambo hiyo ya kisasa ya mawasiliano ya kuongoza ndege kutaruhusu usikuvu na kusikilizana vizuri kati ya Marubani na waongoza ndege.
Johari ametoa ujumbe huo wakati wa kupokea makontena tisa yaliyobeba mitambo ya mawasiliano ya kuongozea kutoka nchi za Norway na Italy mitambo itakayofungwa kwenye viwanja mbalimbali ikiwemo kiwanja cja kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA),Mwanza,Dodoma,Pemba,Unguja,Tabora,Songwe,Tanga,Arusha,Mtwara, Kilimanjaro na Kigoma.
Mradi huo wa Kuboresha mawasiliano ya sauti kati ya Rubani na waongozaji ndege,unatekelezwa Kwa miezi 18 ambao unagharimu shilingi bilioni 31.5 ukihusisha ufungaji wa radio za kidigitali za masafa ya juu,mitambo ya kurekodi pamoja na mifumo ya kuunganisha na kuangalia mawasiliano.
Nae Mkurugenzi wa huduma za uongozwaji ndege kutoka TCAA Flora Mwanshinga anasema mitambo hiyo inauwezo wa kunasa mawasiliano ya sauti Kwa kiwango cha hali ya juu hatua inayochochea safari nyingi za mashirika ye ndege kuruka katika anga la Tanzania hivyo itasaidia kusisimua au kuimarisha uchumi.
Tayari TCAA imeshapeleka wataalum 24 katika nchi za Norway na Italy Kwaajili ya kupata mafunzo ya mitambo hiyo ya kisasa ya mawasiliano ya kuongoza ndege kati ya Rubani na waongozaji ndege.