Zaidi ya watoto 200,000 wamenyanyaswa kingono na makasisi wa Kikatoliki nchini Uhispania tangu 1940, kulingana na matokeo yaliyochapishwa na tume huru mnamo Ijumaa (Oct 27).
Hakuna takwimu maalum iliyotajwa na ripoti hiyo, lakini ilisema kwamba katika kura ya maoni ya watu karibu 8,000 iligunduliwa kuwa asilimia 0.6 ya karibu watu milioni 39 wanaoishi Uhispania walisema walinyanyaswa kijinsia na makasisi wakati walikuwa katika umri mdogo.
Asilimia hiyo iliongezeka hadi asilimia 1.13, na kuifanya kuwa karibu zaidi ya watu 400,000, baada ya unyanyasaji wa waumini kujumuishwa, alisema mchunguzi wa kitaifa wa Uhispania Angel Gabilondo, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ambao uliitishwa kuwasilisha matokeo ya ripoti hiyo.
Ufichuzi uliotolewa nchini Uhispania ni wa hivi karibuni zaidi ambao umetikisa Kanisa Katoliki baada ya kashfa nyingi za unyanyasaji wa kingono kufichuliwa kote ulimwenguni, ambazo kwa ujumla zinahusisha watoto, katika miaka 20 iliyopita.
Ripoti hiyo imekosoa tabia ya Kanisa Katoliki na kuitaka kujibu kesi za unyanyasaji wa watoto zinazohusisha makasisi ”
Ripoti hiyo iliomba kuundwa kwa hazina ya serikali kwa ajili ya kulipa fidia kwa waathiriwa.