Vladimir Putin amepoteza “angalau brigdade” ya wanajeshi katika harakati zake za kukera kuelekea mji wa Avdiivka wa Ukraine, rais Volodymyr Zelensky alisema.
“Wavamizi walifanya majaribio kadhaa ya kuzunguka Avdiivka, lakini kila wakati askari wetu waliwazuia na kuwarusha nyuma, na kusababisha hasara chungu.
Katika visa hivi, adui alipoteza angalau kikosi chake, “Zelensky alisema.
Urusi ilifanya upya mashambulizi katika mji huo uliozingirwa katikati ya mwezi wa Oktoba, ikijaribu kuziba nafasi za Ukraine kwa misururu ya mara kwa mara ya mizinga na mawimbi ya askari na magari ya mapigano, kulingana na mamlaka za mitaa na kijeshi nchini Ukraine.
Brigedi zinatofautiana kwa ukubwa na zinaweza kuwa na askari kati ya 1,500 na 8,000.
Hasara katika uwanja wa vita ni siri ya serikali nchini Urusi na Ukraine, ingawa inaaminika kufikia makumi ya maelfu ya pande zote mbili tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi kamili wa Ukraine mnamo Februari 2022.