Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen ambaye amefariki jana Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa Hospitali akipatiwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa Jumatatu October 30,2023 nyumbani kwake Olosiva Jijini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa, ibada ya kuuaga mwili wa Zelothe itafanyika kesho October 28,2023 saa nne asubuhi nyumbani kwake Sea View Upanga tayari kwa safari ya Arusha ambapo kwa sasa maombolezo yanaendelea Sea View na Arusha.
Nafasi ambazo Zelothe amewahi kutumikia enzi za uhai wake ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamanda wa Polisi Mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma pia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha.