Kwa mujibu wa jeshi la Israel, takriban watu 239, wakiwemo watoto wadogo na wazee, walichukuliwa mateka na Hamas tarehe 7 Oktoba.
Zaidi ya wiki tatu baada ya mashambulizi ya kustaajabisha ya kuvuka mpaka dhidi ya jamii za Israel za kibbutz, miji na kambi za jeshi karibu na mpaka wa Gaza, familia za mateka kwa mara nyingine tena zimetoa wito wa kurejeshwa kwa wapendwa wao.
Baadhi yao wanaunga mkono uvamizi wa Israel huko Gaza, huku wengine wakitetea kubadilishana wafungwa.
Familia za watu waliotekwa na Hamas, kama ilivyo kwa AFP, wanahisi ndio kwanza wanaanza kuchukuliwa kwa uzito na mamlaka. Haya yanajiri huku jamaa za mateka 80 walipokutana na Rais Isaac Herzog siku ya Jumapili.